Latest News


More

MCHUNGAJI LAMECK BYONGE AENDESHA IBADA YA JUMAPILI MWENGE

Posted by : Tumaini Kichila on : Tuesday, May 7, 2013 0 comments
Tumaini Kichila
 Jumapili hii Mchungaji Lameck aliendesha Ibada katika Usharika wa K.K.K.T Mwenge .Katika ibada hiyo ambayo ilikua pia na Ushirika wa Chakula cha Bwana mchungaji Lameck alisaidiana na mchungaji kiongozi wa Usharika wa Mwenge mchungaji Kaanasia Msangi.Mchungaji Lameck Byonge pia ni chaplain wa shule ya kanisa la K.K.K.T Kisarawe
Pichani juu mchungaji Byonge akihubiri kwenye ibada hiyo
 Baadhi ya waumini wakiwa kwenye ibada hiyo.Pichani mbele ni Mama Chacha na mama Palangyo ambao pia ni wazee wa kanisa wa usharika wa Mwenge na pia walikua wazee wa zamu katika ibada hiyo.Pembeni mwa mama Palangyo ni mzee Mushi ambaye pia ni mzee wa kanisa wa Usharika huo
Pichani juu na chini  Waumini wakifuatilia mahubiri katika ibada hiyo Waimbaji wa kwaya kuu wakiimba kwenye ibada hiyo.Katikati aliyevaa joho jeupe ni mchungaji kiongozi Kaanasia Msangi ambaye pia ni mwimbaji wa kwaya kuu
Waimbaji wa kwaya kuu ya Usharika wa Mwenge wakiimba mbele ya Washarika ibadani siku hiyo.Anayeongoza ni mwaliku mkuu wa kwaya hiyo mwalimu Kayese

No comments:

Leave a Reply